Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia, mfano: Chongo, mpiga ghushi, muongo, na mfano wa hayo katika sifa mbaya, hata kama sifa hizo anazo. Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.