Anatueleza sisi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuna baadhi ya watu huwa hawafikirii wanapotaka kuzungumza, je maneno haya nitakayoyazungumza ni ya kheri au la?. na matokeo yanakuwa huyu mzungumzaji anatumbukia kwasababu ya kutofikiria mambo ya haramu, na anaitia nafsi yake katika adhabu ya Mwenyezi Mungu katika moto wa jahanamu, -Mwenyezi Mungu atukinge- na huenda akaporomoka katika moto masafa marefu umbali wa masafa kati ya mashariki na magharibi.