explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- moja ya sababu ambazo hutia nguvu mahusiano kati ya waumini na hueneza mapenzi baina yao, nako ni kuwa mtu atakapompenda ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa mapenzi ya dhati yanayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa ajili ya masilahi ya kidunia.
  • Inapendeza na ni sunna kumueleza anayependwa kwa ajili ya Allah, ili kuongeza mapenzi na kuzoeana.
  • Kuenea kwa mapenzi baina ya waumini hutia nguvu udugu wa kiimani na huhifadhi jamii kuto pasuka na kufarakana.