explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa nguvu halisi si nguvu za mwili,au yule anayemdondosha mwenzake katika wenye nguvu, bali mwenye nguvu na mkali ni yule aliyepambana na nafsi yake na akaitenza nguvu wakati hasira inapokuwa kali; kwa sababu hili linaonyesha uwezo wa nguvu za kuidhibiti nafsi yake na kumshinda kwake Shetani.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Fadhila za upole na kudhibiti nafsi wakati wa hasira, nakuwa hili ni katika matendo mema ambayo uislamu umeyahimiza.
  • Kupambana na nafsi wakati wa hasira ni zaidi ya kupambana na adui.
  • Uislamu umebadili mtazamo wa nguvu wa enzi za ujinga kuwa ni tabia njema, hivyo, mtu mwenye nguvu zaidi kuliko wote ni yule mwenye kumiliki uongozi wa nafsi yake.
  • Kujiweka mbali na hasira; kwani husababisha madhara kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima kwa ujumla.