Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha ukweli, na akasema kuwa kushikamana nao kunapelekea katika matendo mema ya kudumu, na mwenye kushikamana na kufanya wema humpeleka mtendaji wake Peponi, na ukweli wake unapoendelea mara kwa mara kwa siri na hadharani, basi hustahiki jina la mkweli; nayo ni sifa ya hali ya juu zaidi ya ukweli. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaonya dhidi ya kusema uongo na kusema maneno ya batili; Kwa sababu inawachochea watu kuacha uadilifu, na kufanya maovu, ufisadi, na dhambi, kisha inawapeleka Motoni, na anapoendelea kukithirisha kusema uongo basi mpaka huandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa waongo.