Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alimtuma yeye ili akamilishe mambo bora na tabia zilizo njema; kiasi kwamba alitumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili atimize yale waliyokuwa nayo Mitume, na alikuja kukamilisha tabia njema za waarabu, kwani walikuwa wakipenda kutenda kheri na wakichukia shari, walikuwa ni watu wenye utu na ukarimu na utukufu; akatumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili kukamilishe mapungufu yaliyoko katika tabia zao, kama kujifaharisha kwao kwa nasaba, na kujikweza na kumdharau fakiri na nyinginezo.