Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake wakati akihutubia, na ikawa miongoni mwa yale aliyosema ni: Hakika Mwenyezi Mungu amemteremshia wahyi ya kwamba ni wajibu kwa watu wanyenyekeane wao kwa wao, na hii ni kwa kushusha mbawa (kujishusha) kwa viumbe na kuwa wapole, mpaka asijikweze kwa kudai ukubwa na kiburi na utukufu yeyote kwa ukoo wake au mali yake au kinginecho juu ya yeyote, na wala asidhulumu na asifanye uadui yeyote kwa mwenzake.