explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katazo la kuzungumza kuhusu heshima za waislamu.
  • Malipo huendana na matendo, atakayeirudisha heshima ya ndugu yake Mwenyezi Mungu naye atauzuia moto kwake.
  • Uislamu ni dini ya udugu na kuteteana kati ya waislamu.