Aliulizwa Mtume rehema na amani zimfikie: Ni jambo lipi katika Uislamu ni bora? Akataja mambo mawili: La kwanza: Kukirithirisha kuwalisha masikini, na inaingia hapa sadaka na zawadi na kuwakirimu wageni na walima (harusi), na inatiliwa mkazo fadhila ya kulisha masikini katika nyakati za njaa na wakati wa bidhaa kupanda bei. La pili: Kumpa salamu kila muislamu, unayemjua na usiyemjua.