Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.