explain-icon

Ufafanuzi

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake aache kuwa na aibu sana! akambainishia kuwa haya ni katika imani, nakuwa huwa haiji ila kwa kheri. Na haya ni tabia inayomsukuma mtu kufanya zuri na kuacha baya.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kinachokuzuia kufanya kheri hakiitwi kwa jina la haya, bali kitu hicho kinaitwa uoga na kushindwa na kufeli na hofu.
  • Kumuonea haya Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakuwa kwa kufanya maamrisho, na kuacha maharamisho.
  • Kuwaonea haya viumbe kunakuwa kwa kuwaheshimu, na kumpa kila mtu nafasi yake, na kuyapuke yanayotia dosari siku zote.