explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake, Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake. Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine. Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Zimebainishwa baadhi ya sifa zinazopelekea mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, nazo ni uchamungu na unyenyekevu na kuridhika na yale aliyoyagawa Mwenyezi Mungu.