Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wanaohukumu kwa uadilifu na haki baina ya watu walio chini ya utawala wao na hukumu zao, na familia zao, nikuwa watakaa katika makao ya juu zaidi yaliyoumbwa kwa nuru, ikiwa ni takrima kwao siku ya Kiyama. Na mimbari hizi ziko kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake miwili Mtukufu yote ni kulia.