explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama katika kauli na matendo ni tabia njema, na hii ni kwakuwa na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi, na kutenda wema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mtu muovu katika kauli zake na vitendo, mwenye mdomo mchafu katika yale yanayotamkwa na ulimi wake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ubora wa tabia njema; kwa sababu humletea mwenye nayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na mapenzi ya waja wake, nalo ndilo jambo kubwa katika yale yatakayopimwa siku ya Kiyama.