explain-icon

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi kimeangamia kipandwa changu, nipe msaada, na unipe kipandwa kitakachonifikisha, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa udhuru yakuwa yeye hana kitu cha kumsaidia, mtu mmoja akasema na alikuwepo katika mazungumzo: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuelekeza kwa mtu atakaye mbeba, akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atashiriki katika kupata malipo na mtoaji, kwa sababu amemuelekeza muhitaji kwake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kuelekeza katika kheri.
  • Himizo la kufanya kheri ni katika sababu za kuinyanyua jamii ya kiislamu na kutoshelezana.
  • Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Hadithi hii ni kanuni kuu, yanaingia hapa matendo yote ya kheri.
  • Mtu atakaposhindwa kutimiza hitajio la muombaji, basi amuelekeze kwa mwingine.