explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa upole na ulaini na utaratibu katika kauli na matendo huyazidishia mambo uzuri na ukamilifu na ubora, na mtu mwenye sifa hizi hakika anastahiki kupata hitajio lake. Na kukosekana kwa upole huyatia aibu mambo na kuyatia sura mbaya na humkwamisha mtu kupata shida yake, na hata akiipata huipata kwa tabu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kujipamba na upole.
  • Upole humpamba mtu, nayo ni sababu ya kila heri katika mambo ya Akhera na Dunia.