Alinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha mapenzi, kama alichopata Ibrahim -Amani iwe juu yake-, na kwa ajili hiyo alikanusha kuwa na mwandani zaidi ya Allah; Kwa sababu moyo wake umejaa mapenzi ya Allah Mtukufu na kumtukuza kwake na kumtambua kwake, hivyo hauwezi kupata nafasi kwa yeyote zaidi ya Allah, Na lau kama angelijifanyia mwandani katika viumbe basi angelikuwa ni Abubakari. Kisha akatahadharisha kwa kuchupa mipaka inayofaa katika mapenzi kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao na wema wao mpaka wakayageuza kuwa miungu ya kishirikina inayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na wakajenga juu ya makaburi yao misikiti na mahekalu, na akaukataza -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake wasijekufanya mfano vitendo vyao.