Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na idadi yao walikuwa kumi, akawaunga mkono tisa miongoni mwao juu ya Uislamu na kufuata sheria, na hakumuunga mkono wa kumi, alipoulizwa kuhusu sababu yake, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo kavaa hirizi, nayo ni kila kinachotundikwa, ikiwemo shanga na vinginevyo kwa lengo la kuzuia kijicho au madhara. Yule bwana akaingiza mkono wake mahali ilipo hirizi na akaikata na akaepukana nayo, hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuunga mkono, na akasema akitahadharisha kuhusu hirizi na akibainisha hukumu yake: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya shirki".