Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.