Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu. Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.