Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.