Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwatuma Masahaba wake wasiache "Sanamu" nayo ni picha ya kiumbe hai yenye kiwiliwili- isipokuwa wameliondoa au kuifuta. Na wasiache kaburi lililonyanyuka ila wamelisawazisha na ardhi, na wayabomoe yaliyomo katika majengo, au walisawazishe lisinyanyuliwe sana kupita usawa wa ardhi, bali linyanyuliwe kiasi cha shibri moja (kipimo cha kiganja).