Alitoa habari Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu atamchagua mtu katika umma wake kwenye kundi la watu siku ya Kiyama atamuita ili amuhesabu, basi atamtolea mafaili tisini na tisa na mafaili hayo ni ya matendo yake mabaya ambayo alikuwa akiyafanya Duniani, na urefu wa kila faili ni mfano wa upeo wa macho, Kisha Mwenyezi Mungu atamwambia mtu huyu: Je unapinga chochote katika haya yaliyoandikwa katika mafaili? Je Malaika wangu wenye kuhifadhi wanayoandika wamekudhulumu? Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Je una chochote cha kujitetea nacho katika matendo yako uliyoyatanguliza miongoni mwa matendo ya Duniani?katika matendo uliyoyafanya kwa kusahau au kwa kukosea au kwa kutojua, Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu sina chochote cha kujitetea nacho. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Si hivyo, kwa hakika wewe una mambo yaliyoandikwa kwetu sisi, na kwa hakika wewe hutodhulumiwa leo hii. Akasema: Basi itatolewa kadi iliyoandikwa ndani yake: Ash-hadu An-laa ilaaha illa llaah wa Ash-hadu Anna Muhammadan Ab-duhuu wa Rasuuluhu. Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Angalia Mizani yako. Basi atasema mtu yule hali ya kuona ajabu: Ewe Mola wangu! ni uzito wanini huu wa kikadi kidogo pamoja na kupimwa na mafaili yote haya? Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hautadhulumiwa leo hii. Akasema: Basi mafaili yatawekwa katika sehemu ya kupimia, na Kadi kwenye sehemu nyingine ya kupimia; Hivyo basi ukawa mwepesi upande wa kupimia palipo na Mafaili na ukawa mzito upande wa kupimia palipo na Kadi, hivyo basi Mwenyezi Mungu akamsamehe.