explain-icon

Ufafanuzi

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa siku ya Kiyama yeye atakuwa kwenye Birika lake ili amuone kila mwenye kuja kwenye Birika katika watu wa umma wake. Na watachukuliwa watu wakiwa karibu na Mtume -Amani iwe juu yake- basi atasema: Ewe Mola wangu hao ni wangu na nikatika umma wangu, Basi kutasemwa: Je unajua walichofanya baada ya wewe kuachana nao? Namuapia Mwenyezi Mungu hawakuwacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao, hivyo basi hao siyo watu wako wala si katika umma wako.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Huruma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kwa umma wake na kuwatilia umuhimu.
  • Hatari ya kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake.
  • Himizo la kushikamana na sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake.