Anawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni: Chongo wa jicho. Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho. Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.