Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.