explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu waovu, nakuwa hao ndio Kiyama kitasimama juu yao, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa misikiti, wakisali hapo na wakiyaelekea wakati wa ibada.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi; kwa sababu kitendo hicho ni njia ya kuingia katika shirki.
  • Uharamu wa kusali katika makaburi hata bila kujengea; kwa sababu msikiti ni jina la kila mahali panaposujudiwa hapo hata kama hakuna jengo.
  • Atakayeyafanya makaburi ya watu wema kuwa mahala pa kusalia huyo ni katika viumbe waovu, hata kama atadai kuwa lengo lake ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.