Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema kuwa dini hii itaenea sehemu zote za ardhi, hivyo dini hii itafika sehemu yoyote ile ufikapo usiku na mchana, na hatoiwaacha Mwenyezi Mungu Mtukufu nyumba yoyote mijini na vijijini wala mabondeni na majangwani isipokuwa ataiingiza dini hii, atakayeikubali dini hii na akaiamini basi atakuwa mtukufu kwa sababu ya utukufu wa Uislamu, na atakayeikataa na akaipinga basi atakuwa dhalili mwenye kufedheheshwa. Kisha swahaba Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akaeleza kuwa alilijua hilo aliloambiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kwa watu nyumba yake hasa, kwani kila aliyesilimu miongoni mwao alipata kheri na heshima, na utukufu, na aliyekufuru miongoni mwao alipata udhalili na unyonge, hii ikiwa ni pamoja na pesa anazowalipa Waislamu kama Jizia (Kodi).