explain-icon

Ufafanuzi

Ametueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayempa muda mdaiwa wake au akampunguzia katika deni lake, basi malipo yake: Nikuwa Allah atampa kivuli siku ya Kiyama ambayo jua litasogea karibu na vichwa vya waja na joto lake litakuwa kali mno, Hatopata yeyote kivuli isipokuwa atakayetiwa kivuli na Mwenyezi Mungu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Fadhila za kuwafanyia wepesi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hilo ni katika sababu za kuokoka na misukosuko ya siku ya Kiyama.
  • Malipo huenda sawa na matendo.