Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa: La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini? La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki? La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?. La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?