Walikuwa Masahaba pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usiku mmoja akatazama katika mwezi (Usiku wa terehe kumi na nne (14), akasema: Hakika waumini wote watamuona Mola wao Mlezi kwa hakika kabisa kwa macho bila kutatizika, nakuwa hawatosukumana na wala hawatopata tabu wala uzito wakati wa kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ikiwa mtaweza kuzizuia sababu ambazo zinakuzuieni kuto swali swala ya Alfajiri na swala ya Alasiri basi fanyeni hivyo, na zitekelezini kikamilifu ndani ya wakati wake na katika jamaa, kwani hilo ni miongoni mwa sababu za kuuona uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake- Aya "Na utakase sifa za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake"