Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kutumbukia katika dhuluma ya ndugu yake Muislamu katika heshima, au mali, au damu, basi amuombe aliyemdhulumu amsamehe madamu bado yuko Duniani, kabla haijafika siku ya Kiyama, kiasi ambacho Dinar ya dhahabu wala Dirham ya fedha haitofaa kitu kwa kumlipa aliyemdhulumu ili aikomboe nafsi yake; kwani kisasi siku hiyo kitakuwa kwa matendo mema na mabaya; kiasi kwamba aliyedhulumiwa atachukua kutoka katika mema ya aliyemdhulumu kwa kiwango cha dhuluma yake alichodhulumiwa, ikiwa dhalimu hatokuwa na mema basi yatapunguzwa maovu ya aliyedhulumiwa na kubebeshwa dhalimu kwa kiwango cha dhuluma yake.