explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa jambo la kwanza litakalohukumiwa baina ya watu katika dhulma zao wao kwa wao siku ya Kiyama: Itakuwa katika damu, kama kuua na kujeruhi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ukubwa wa swala la damu, kwani siku zote jambo muhimu zaidi ndio hutangulizwa.
  • Dhambi huwa kubwa kulingana na madhara yanayojitokeza, na kuua nafsi isiyo na hatia ni katika madhara makubwa na hakuna kubwa zaidi yake isipokuwa ukafiri na kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.