Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Jua litasogezwa siku ya Kiyama karibu na viumbe, mpaka liwe vichwani mwao kwa kiasi cha maili moja. Amesema taabii (Mwanafunzi wa swahaba) Saidi bin Aamiri: Wallahi sijui ni maili mbili zipi alikusudia, je ni masafa ya ardhi, ama ni maili (wanja) ambao hutumika kupaka macho? Akasema: Watakuwa katika jasho kulingana na amali zao; yuko miongoni mwao ambaye jasho lake litatiririka mpaka chini ya kongo mbili zake za miguu, na yuko ambaye jasho lake litatiririka mpaka magotini, na yuko ambaye jasho litakuwa katika kitovu chake na kiunoni kwake, na yuko ambaye jasho litafika katika mdomo wake na litamzuia kuzungumza. Amesema: Na akaashiria rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake katika kinywa chake.