Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba zake: Je, mnamjua aliyefilisika? Wakasema: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule asiye na fedha wala mali. Akasema: Aliyefilisika katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule anayefanya mambo mema kama Swala, Saumu na Zaka, na akaja akiwa kamshutumu huyu na kamtukana huyu, na kamsingizia mabaya mtu huyu katika heshima yake, na kala mali ya huyu na akakana, na akamwaga damu ya huyu na kumdhulumu, na kampiga huyu na akamdhalilisha, hivyo mtu aliyedhulumiwa atapewa kutoka katika matendo yake mema, mema yake yakimalizika kabla ya haki za watu na dhulma hazijamalizika, yatachukuliwa madhambi ya wale aliowadhulumu na kuwekwa katika vitabu vya dhalimu, kisha atatupwa na kurushwa motoni kwani hajabaki na jema.