Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kundi la kwanza la waumini watakaoingia peponi nyuso zao zitakuwa na sura ya mwezi unapokuwa usiku wa tarehe kumi na tano katika mg'ao, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali yenye mng'ao na mwangaza katika mbingu, watakuwa na sifa za ukamilifu kiasi kwamba hawatokojoa, wala kujisaidia haja kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao ni vya dhahabu, na jasho lao ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vinafuka hurufu nzuri mno, na udi mzuri zaidi, na wake zao watakuwa ni Mahurulaini, umbile lao litakuwa kama umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam katika urefu na umbile; ulikuwa urefu wa mwili wake ni dhiraa sitini kwenda juu.