Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana: "Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu" nayo ni matamshi ambayo hutumika kuita katika ibada ya Mwenyezi Mungu na swala, "Uliotimia" uliokamilika, wito wa tauhidi na ujumbe, "na swala iliyosimama" yenye kudumu ambayo itasimamishwa hivi punde, "mpe" mgawie, "Muhammadi utetezi" na cheo cha juu peponi ambacho hakimstahiki mwingine ila yeye rehema na amani ziwe juu yake, "na fadhila" cheo cha juu zaidi ya vyeo vya viumbe, "na umfufue" na umpe "nafasi yenye kusifiwa" anayosifiwa mwenye kuwanayo; nao ni utetezi mkuu wa siku ya Kiyama, "uliyomuahidi" kwa kauli yako "Huenda akakufufua Mola wako katika nafasi yenye kusifiwa" ili iwe yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Atakayeomba dua hii atastahiki kuupata utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.