Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sifa za watu wa peponi na za watu wa motoni. Asilimia kubwa ya watu wa peponi ni: "Kila mnyonge mwenye kujishusha", yaani: Mnyenyekevu mwenye kujishusha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwenye kuidhalilisha nafsi yake kwake, mpaka baadhi ya watu wakamdhoofisha na kumdharau, na huyu mwenye kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lau kama ataapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha kutamani jambo katika karama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu angemuepusha na kutopokea kiapo chake, na angelimtimizia alichokiapia na angelijibu ombi lake na dua yake. Na asilimia kubwa ya watu wa motoni ni: Kila "Mkaidi" Naye ni fidhuli mkorofi mwingi wa ugomvi, au muovu asiyetii kwa kufata jambo la kheri, "Jeuri" Naye ni mwenye kiburi, mlafi, mwenye mwili mkubwa, mwenye kutembea kwa maringo, mwenye tabia mbaya, "Mwenye kufanya kiburi" kwa kuikataa kwake haki, na kwa kumdharau mtu mwingine.