Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akishitakia kuhusu matendo ya Watumwa wake, Watumwa hao wanamdanganya na kumfanyia hiyana katika amana, na wanafanya ghushi katika miamala, na wanakwenda kinyume na maelekezo yake, naye huwatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo akaulizia kuhusu hali yake itakavyokuwa siku ya Kiyama, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Watahesabiwa kwa kile walichokufanyia hiyana na kwenda kinyume na maelekezo yako na kukudanganya na wewe utahesabiwa ulivyo waadhibu, basi ikiwa adhabu uliyowapa itakuwa sawa na makosa yao basi hutokuwa na kosa lolote, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ndogo ikilinganishwa na kosa walilofanya basi ni jambo zuri utalipwa na utazidishiwa katika malipo yako, na ikiwa adhabu uliyowapa ni zaidi ya walichokifanya, basi utaadhibiwa na malipo yako uliyozidishiwa yatachukuliwa na watapewa wao, basi yule bwana akakaa pembeni akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote, hata kama jambo hilo litakuwa na uzito sawa na punje ya Hardal tutalileta Nasi tunatosha kuwa wajuzi wa hisabu" (Al-Anbiyaa 47), hivyo basi hatodhulumiwa mtu yoyote siku ya kiyama, na kipimo cha watu kitakuwa cha uadilifu, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na wao zaidi ya kuwaacha huru ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia hivi sasa wako huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kwa kuogopea hesabu na adhabu.