Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mauti yataletwa siku ya Kiyama, kwa mfano wa dume la kondoo lilochanganya rangi nyeupe na nyeusi, Basi ataita mwenye kuita: Enyi watu wa peponi! Basi watainua shingo zao na watainua vichwa vyao na wataangalia, Basi atawaambia: Je mnamjua huyu? Basi watasema: Ndiyo haya ni mauti, na wote kwa hakika wameyaona na kuyajua, Kisha muitaji ataita: Enyi watu wa Motoni, na watainua shingo zao na vichwa vyao na wataangalia, Basi atasema: Je mnamjua huyu? Hivyo watamjibu: Ndiyo, haya ni mauti, na wote wameyaona; Basi atachinjwa, kisha atasema mwenye kuita: Enyi watu wa peponi bakieni humo milele na hakuna kufa, na enyi watu wa Motoni bakieni humo milele na wala hakuna kufa, Na kumefanywa hivyo ili iwe ni ziada ya neema kwa waumini, na iwe ni adhabu yenye kuumiza kwa makafiri. Kisha akasoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa, nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" Hivyo basi siku ya Kiyama watatenganishwa watu wa Peponi na watu wa Motoni, na wataingia wote kule walipopangiwa na kukaa humo milele, Basi atajuta mkosaji atapata mshituko na kujuta kwa nini hakufanya mema, na mwenye matendo machache pia kwa nini hakuzidisha mambo ya heri.