Atakayetoa sadaka kwa vitu viwili katika vitu vyovyote, mfano kama vyakula au mavazi au kipando au pesa, kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu humuita Malaika katika milango ya pepo wakimkaribisha kuelekea katika milango hiyo, nao wakisema: Hakika umetanguliza kheri nyingi unalipwa kwazo leo malipo makubwa. Wale wenye kukithirisha swala wataitwa katika mlango wa swala, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha sadaka wataitwa katika mlango wa sadaka, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha kufunga Malaika watawapokea katika mlango wa Rayyan wakiwaita kuingia hapo, na maana ya Rayyan: ni mtu anayekata kiu; kwasababu wafungaji hujizuia na kunywa maji wakapatwa na kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi kirefu na chenye joto, hivyo watalipwa kwa kiu yao kwa kukatwa kiu milele katika pepo ambayo wataingia kupitia mlango huo. Aliposikia Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake- mazungumzo haya, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, "fidia yako namtoa baba yangu na mama yangu" atakayeingia katika milango hii hatokuwa na mapungufu wala hasara, kisha akasema: "Je inawezekana mtu akaitwa katika milango hiyo yote?" Akasema -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, na ninataraji wewe kuwa miongoni mwao".