Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].