Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunadi atanadi kuwaita watu wa peponi wakiwa humo wakineemeka: Hakika leo hii mtapata afya na hamtaugua peponi kamwe, kwa namna yoyote ile yatakavyokuwa madogo maradhi hayo, na hakika mtapewa uhai wala hamtakufa humo milele hata usingizi pia hamtaupata ambao ndio kifo kidogo, na leo mtaishi humo mkiwa vijana na wala hamtozeeka humo milele, nakuwa mtaneemeka humo wala hamtohuzunika milele, na hiyo ni kauli yake Mtukufu: "Na wataitwa (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].