Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele". Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Peponi wakiwa humo: Enyi watu wa Peponi, nao watamjibu kwa kusema: Labeka, tumekuitikia Mola wetu Mlezi! na utukufu ni wako, Atasema kuwaambia: Je! mmeridhika? Watasema: Ndiyo, tumeridhika; Kwa nini tusiridhike wakati umetupa ambacho hukumpa kiumbe wako yeyote! Atasema Mtukufu: Je, nisikupeni kilicho bora kuliko hicho? Watasema: Ewe Mola Mlezi, na ni kitu gani kilicho bora kuliko hicho? Atasema: Ninakuteremshieni juu yenu radhi zangu daima; na sitokukasirikieni baada yake milele.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Mazungumzo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na watu wa peponi.
  • Habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wa peponi ya kuwaridhia, na kuwateremshia radhi juu yao na kutochukia tena milele.
  • Kila mtu Peponi ataridhika na hali yake licha ya kutofautiana viwango vyao na kupishana daraja zao; Kwa sababu wote walijibu kwa neno moja, ambalo ni: "Umetupa kile ambacho hukumpa yeyote katika viumbe vyako."