explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili: Uchamungu na tabia njema. Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake. Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero. Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni: Ni ulimi na utupu. ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo. Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kuingia peponi kuna sababu zake ambazo zinaambatana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kumcha yeye, na sababu zinazohusiana na watu, kama: Tabia njema.
  • Hatari ya ulimi kwa mtu, nakuwa ni katika sababu za kuingia motoni.
  • Hatari ya matamanio na machafu kwa mwanadamu, nakuwa hayo ni katika sababu kubwa za kuingia motoni.