Alimueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na akamridhia kuwa Mola na Mungu na mmiliki na mtukufu na muamrishaji, na Uislamu kuwa ni dini, kwa kutii na kujisalimisha katika amri zake zote na makatazo yake yote, na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii, kwa yote aliyotumwa kwayo na akayafikisha; itamthibitikia kwake Pepo, Abuu Saidi akastaajabu radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Yarudie tena ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akafanya hivyo, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na nina jambo jingine ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu humnyanyua mja daraja mia moja Peponi kwalo, masafa yaliyoko kati ya daraja mbili hizo ni kama umbali ulioko baina ya mbingu na ardhi, akasema Abuu Saidi: Na nilipi hilo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.