Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa amali njema ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi Dhul-Hija ni bora kuliko siku zingine. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kupigana Jihadi katika siku kumi hizi, je ni bora au kufanya matendo mema katika siku hizi? Kwakuwa linajulikana kwao kuwa Jihadi ni amali bora. Akajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Yakuwa amali njema ndani ya siku hizi ni bora kuliko Jihadi katika siku zingine, isipokuwa mtu aliyetoka Jihadi na akaihatarisha nafsi yake na mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, akapoteza mali yake na ikatoka roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hiki ndicho kilicho bora kuliko amali njema ndani ya siku hizi bora.