Alisimama Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kati ya maswahaba kwaajili ya kuwahutubia, akawaeleza kuwa kupigana jihadi kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu na kumuamini Mwenyezi Mungu ndiyo matendo bora, akasimama bwana mmoja akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hivi unaonaje kama nitauwawa kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu je nitasamehewa mimi madhambi yangu?, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, lakini kwa sharti uwe umeuwawa ukiwa na subira na uvumilivu kwa yale yaliyokupata, ukitakasa nia kwaajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bila kukimbia kiwanja cha vita, kisha akakumbuka Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kitu, nacho ni deni, akakumbusha kuwa jihadi na shahada havifuti haki za wanadamu.