explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji. Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hili ni himizo kwa waislamu kusaidizana katika heri.
  • Amesema bin Hajar: Katika Hadithi hii kuna himizo la kuwafanyia wema wale wanaowafanyia wema Waislamu, au kutekeleza moja ya wajibu wao.
  • Kanuni ya jumla nikuwa: Yeyote anayemsaidia mtu katika kumtii Mwenyezi Mungu atapata malipo sawa na malipo yake, bila ya kupunguzwa ujira wake hata kidogo.