explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Nia ya dhati na kufanya linalowezekana ni sababu ya kupata thawabu na malipo yaliyokusudiwa, hata kama amali inayotakiwa haijatekelezwa.
  • Himizo la jihadi na kuomba shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umma huu, kwani anaupa kupitia amali ndogo daraja za juu zaidi peponi.